URUSI-CORONA-AFYA

Wagonjwa wa Corona wapindukia 272,043 nchini Urusi

Visa vingi vya maambukizi vyaendelea kushuhudiwa nchini Urusi.
Visa vingi vya maambukizi vyaendelea kushuhudiwa nchini Urusi. REUTERS/Tatyana Makeyeva

Urusi imerekodi visa 272,043 vay maambukizi ya virusi vya Corona bada ya visa vipya 9,200 kuthibitishwa, kituo cha kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Corona nchini hmo kimetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Urusi imethibitisha visa vipya 119, na kufanya idadi watu 2,537 ambao wamepoteza maisha, kwa jumla ya visa 272,043 maambukizi chini humo, na wagonjwa 63,116 wamepona ugonjwa huo.

 

Idadi ya vifo vilivyotokana na maambukizi ya virusi vya Corona duniani kote imepindukia watu 307,000, ambapo vingi vya vifo hivyo vimetokea Ulaya na Marekani, tangu kuzuka kwake huko China, mwishoni mwa mwaka uliopita.

Marekani ndio yenye visa vingi kwa kuwa na vifo 88,237, ikifuatiwa na Uingereza vifo zaidi ya 33,614, Italia vifo 31,610, Ufaransa vifo 27,529 na Uhispania yenye vifo 27,429.

Ulaya bara ambalo limeshambuliwa vikali na virusi, ambapo mataifa kama Italia, Uhispania na Ujerumani ni miongoni mwa mengine 10 ambayo yana idadi kubwa ya maambukizi na vifo. Ujerumani inatarajiwa kuanza kuchukua hatua za kulegeza masharti ya mipakani Jumamosi, wakati mataifa mengine kadhaa ya jirani yatarajaiwa kuichukua hatua kama hizo kuanzia Juni 15. Umoja wa Mataifa umesema janga la corona limesaabisha matatizo ya akili duniani kote.

Mapema wiki hii Mkuu wa Shirika la Afya Duniani kwa Ulaya, Hans Kluge alisema kasi ya usambaaji wa virusi vya corona kwa Ulaya, inapungua, lakini aliongeza kuwa lazima mataifa yaendelea kuwa madhubuti katika kukabiliana na janga hilo.