URUSI-CORONA-AFYA
Coronavirusi: Visa vipya vya maambukizi vyaendelea kupungua nchini Urusi
Urusi imerekodi leo Jumatatu kesi mpya 8,926 za maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya saa 24, na kufanya jumla ya idadi ya maambukizi yaliyothibitishwa nchini humo 290,678 tangu kuzuka kwa janga hilo.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Idadi ya visa vipya vya maambukizi inaendelea kusalia kwenye kiwango cha watu 10,000 kwa siku ya tatu mfululizo.
Kulingana na mamlaka nchini Urusi, ugonjwa wa Covid-19 umewauwa watu wengine 91, na kufanya idadi ya vifo nchini Urusi kufikia 2,722.
Wakati huo huo maambukizi ya virusi vya Corona yamefikia milioni 4.7 ulimwenguni.
Zaidi ya watu 314,000 wamekufa kote ulimwenguni kutokana na COVID-19 na zaidi ya milioni 4.7 wameambukizwa.