Pata taarifa kuu
URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Urusi yakaribia kufikisha idadi ya maambukizi 300,000

Kulingana na kituo cha kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Covid-19, watu 2,837 wamekufa kutokana na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na watu 115 ndani ya saa 24 zilizopita.
Kulingana na kituo cha kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Covid-19, watu 2,837 wamekufa kutokana na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na watu 115 ndani ya saa 24 zilizopita. REUTERS

Urusi imerekodi leo Jumanne visa vipya 9,263 vya maambukizi ya virusi vya Corona na kufanya idadi ya visa vya maambukizi kupindukia karibu 299,941 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya visa vipya kwa kila siku iko chini ya 10,000 kwa siku ya nne mfululizo. Idadi hiyo ilizidi mara kadhaa kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Kulingana na kituo cha kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Covid-19, watu 2,837 wamekufa kutokana na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na watu 115 ndani ya saa 24 zilizopita.

Hayo yanajiri wakati idadi ya visa vya maambukizi duniani imefikia Milioni 4.81 baada ya visa vipya 93, 324 kuthibitishwa, huku wagonjwa Milioni 1.79 wakithibitishwa kupona ugonjwa huo ambao umeua watu 319,000.

Wakati huo huo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamependekeza kuanzishwa kwa mfuko wa euro bilioni 500 wa kufadhili juhudi za kuukwamua uchumi wa nchi za Ulaya zilizoathirika zaidi na janga la Corona.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.