Pata taarifa kuu
INDIA_BANGLADESH-MAJANGA YA ASILI

Kimbunga Amphan chaua watu 84 nchini India na Bangladesh

Kimbunga Amphan kimesababisha uharibifu mkubwa huko Calcutta. Picha hii inaonyesha uharibifu huko Kolkata.
Kimbunga Amphan kimesababisha uharibifu mkubwa huko Calcutta. Picha hii inaonyesha uharibifu huko Kolkata. REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Kulingana na ripoti rasmi iliyotangaza Alhamisi hii, Mei 21, nchini India, "watu 72 wamefariki dunia, ikiwa ni pamoja 15 huko Calcutta," Waziri Mkuu Mamata Barnerjee amewaambia waandishi wa habari.

Matangazo ya kibiashara

Upande wa Bangladesh, polisi na maafisa wameliambia shirika la habari la AFP kwamba watu 12 wamefariki dunia.

Kimbunga Amphan kimeharibu sehemu za Kaskazini Mashariki mwa India na Bangladesh usiku wakuamkia leo Alhamisi.

Nyumba nyingi zimesombwa na maji, huku wakazi wengi wakipoteza mali na vitu.

Miti kadhaa imekatika na kusababisha vifo vya watu wengi, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka serikalini nchini India.

Watu wengi wanahitaji msaada wa dharura katika ghuba ya Bengale na huko Calcutaa, mji wenye wakazi milioni 15.

Watu 500,000 wameanza kuhamishwa katika maeneo salama, kwa mujibu wa vyanzo kutoka idara ya huduma za dharura.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.