CHINA-CORONA-AFYA

Virusi: China yatangaza ushindi dhidi ya Corona, Brazil yaathirika zaidi

Mbele ya wabunge 3,000 waliovaa barakoa, Bw. Li ameelezea "kazi kubwa" ambayo imebaki kutekelezwa katika dhidi ya athari ya virusi kwenye uchumi wa China.
Mbele ya wabunge 3,000 waliovaa barakoa, Bw. Li ameelezea "kazi kubwa" ambayo imebaki kutekelezwa katika dhidi ya athari ya virusi kwenye uchumi wa China. AFP

China imetangaza leo Ijumaa kuwa imepata ushindi dhidi ya ugonjwa wa Corona, ambao umeathiri uchumi wake na unaendelea kushika kasi mahali pengine ulimwenguni, hasa nchini Brazil ambapo ugoj-njwa huo umeua watu zaidi ya 20,000.

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa janga hilo sasa limeathiri zaidi ya watu milioni 5 na kuuwa watu 329,799 duniani kote kulingana na visa vilivyothibitishwa- na kwa kwa baadhi ya takwimu kupindukia - China, ambapo virusi hivyo vilianzia mwishoni mwa mwaka wa 2019, imeweza kudhibiti ugonjwa huo hata kama Marekani inaishutumu kuchelewa kwamba imechukuwa hatua.

"Tumepata mafanikio makubwa ya kimkakati katika vita vyetu dhidi ya Covid-19," ametangaza Waziri Mkuu Li Keqiang siku ya kwanza ya kikao cha Bunge la taifa(PNA), mkutano mkubwa wa utawala wa kikomunisti.

Kwa mara ya kwanza katika historia yake ya hivi karibuni, Beijing imejitolea kuweka lengo la ukuaji kwa mwaka huu, ikishindwa kutoa kiwango cha athari za ugonjwa wa Covid-19.

Mbele ya wabunge 3,000 waliovaa barakoa, Bw. Li ameelezea "kazi kubwa" ambayo imebaki kutekelezwa katika dhidi ya athari ya virusi kwenye uchumi wa China.