SUADI ARABIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Marufuku ya kutotembea kufutwa Juni 21 Saudi Arabia

Barabara Kuu ya King Fahd, moja ya barabara zinazotoka na kuingia Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.
Barabara Kuu ya King Fahd, moja ya barabara zinazotoka na kuingia Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia. Ammar shaker/wikimedia.org

Saudi Arabia inatazamiwa kuanza kulegeza muda wa kuanza kwa shughuli za kawaida wiki hii kabla ya kuondoa marafuku hiyo baadaye. Saudi Arabia imerikodi visa 74,795 vya maambukizi. Wagonjwa 45,668 wamepona na 399 wamefariki baada ya vifo vipya 9 kuthibitishwa.

Matangazo ya kibiashara

Saudi Arabia imetangaza kwamba itaondoa kila aina ya sheria ya kutotembea kuanzia Juni 21 isipokuwa katika jiji takatifu la Makkah, Waziri wa Mambo ya Ndani amesema Jumanne baada ya zaidi ya miezi miwili ya vizuizi kwa kudhibiti ugonjwa wa Covid-19.

Shirika la habari la serikali nchini Saudia, limesema marufuku ya kutotembea itaanza saa tisa jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi, na misikiti itafunguliwa Juni 21.

Ibada zinaweza kuanza tena katika misikiti yote ya nje ya jiji la Makkah kuanzia Mei 21, wizara hiyo imebaini katika mfululizo wa hatua zilizochapishwa na shirika la hhabari la serikali la SPA.

Nchi hii ya Kifalme, ambayo imeathirika zaidi na janga hili miongoni mwa majirani zake wa Kiarabu wa Ghuba, ilitangaza amri ya kutotoka nje kwa siku tano mfululizo nchini kote wakati wa Eid al-Fitr, sikukuu ya Waislamu ambayo inaashiria mwisho wa mwezi wa mfungo wa Ramadhani, uliyoadhimishwa kuanzia Jumapili Mei 24.