Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-USALAMA

Mvutano kati ya polisi na waandamanaji waongezeka Hong Kong

Vikosi vya usalama pia vimezingira watu wengi kwenye mitaa ya eneo la kibiashara katika mji wa Hong Kong na wengine wamepelekwa karibu na jengo la jengo la bunge katika eneo hilo.
Vikosi vya usalama pia vimezingira watu wengi kwenye mitaa ya eneo la kibiashara katika mji wa Hong Kong na wengine wamepelekwa karibu na jengo la jengo la bunge katika eneo hilo. REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Kikosi cha polisi wa kutuliza ghasia huko Hong Kong wametumia gesi ya machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga dhidi ya muswada wa sheria kuhudu usalama wa taifa ambao China inataka kuweka katika eneo hilo linalojitawala.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kumetokea makabiliano makali kati ya waandamanaji na askari wa kikosi cha polisi cha kutuliza ghasia katika eneo la kibiashara la Hong Kong, wakati polisi ilikuwa ikiondoa vizuizi barabarani vilivyokuwa vimewekwa na waandamanaji.

Vikosi vya usalama pia vimezingira watu wengi kwenye mitaa ya eneo la kibiashara katika mji huo na wengine wamepelekwa karibu na jengo la jengo la bunge katika eneo hilo, wakati wanaharakati walitoa wito wa kuandamana kupinga dhidi ya muswada unaolenga kuweka adhabu kali kwa watu ambao hawataheshimu wimbo wa taifa wa China.

Hali hii inakuja wakati mvutano unaendelea kuongezeka kuhusu uheshimishwaji wa uhuru katika koloni hili la zamani la Uingereza.

Maandamano ya wanaharakati wanaounga mkono demokrasia, ambayo yalisitishwa kutokana na kipindi kigumu cha mgogoro wa afya uliyotokana na ugonjwa aw Covid-19, yalianza tena wiki iliyopita huko Hong Kong baada ya kuwasilishwa kwa muswada wa sheria kuhusu usalama wa Beijing.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.