Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-USHIRIKIANO

Baraza la Congress la Marekani latoa wito wa vikwazo dhidi ya maafisa waandamizi wa China

Capitole, makao makuu ya Baraza la Congress, Washington, D.C.
Capitole, makao makuu ya Baraza la Congress, Washington, D.C. REUTERS/Kevin Lamarque
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Baraza la Wawakilishi la Mamrekani limepitisha azimio la kuutaka utawala wa Donald Trump kuweka vikwazo zaidi kwa maafisa wakuu wa China wanaoaminika kuwa ni wahusika wakuu wa ukandamizaji ulioedeshwa dhidi ya Waislamu kutoka jamii ya Uighur katika Mkoa wa Xinjiang nchini China.

Matangazo ya kibiashara

Muswada huo, ambao tayari umepitiswa katika Bunge la Seneti, umepitishwa katika Baraza la Wawakilishi kwa kura 413 dhidi ya moja. Kwa hatua inayofuata, muswada huo utapelekwa kwa rais Donald Trump kwa ajili ya kutiliwa saini.

Azimio hilo linalenga hasa Chen Quanguo, Katibu wa Chama cha Kikomunisti katika Mkoa wa Xinjiang na mjumbe mwenye ushawishi mkubwa katika kamati kuu ya chama (Politburo) ambaye ni mmoja wa wakuu wa utawala wa China. Wajembe kutoka vyama vya Republican na Democratic wanamshtumu kwa "ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu".

Kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa, wati Milioni moja kutoka jamii ya Uighur wamlifungwa katika kambi huko Xinjiang. China imekanusha udhalilishaji wowote dhidi yawatu kutoka jamii ya Uighur na jamii zingine za Waislamu wachache.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.