Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-USALAMA

China: Bunge lapitisha mpango wa sheria mpya ya usalama Hong Kong

Wanaharakati wanaandamana wakipinga mpango wa sheria mpya ya usalama Hong Kong, China, Mei 22, 2020.
Wanaharakati wanaandamana wakipinga mpango wa sheria mpya ya usalama Hong Kong, China, Mei 22, 2020. REUTERS/Tyrone Siu

Bunge la China limepitisha kwa kauli moja mpango wa sheria mpya ya usalama huko Hong Kong, sheria ambayo imeendelea kuzua utata nchini humo na kusababisha maandamano makubwa katika eneo hilo lililokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Bunge limepiga kura kuunga mkono pendekezo la kutungwa sheria hiyo itakayowaadhibu wanaojihusisha na kutaka kujitenga, kudhoofisha nguvu ya dola, ugaidi na vitendo vyote vinavyotishia usalama wa taifa.

Wabunge 3,000 wa bunge la kitaifa la China (PNA) wamepitisha hatua hiyo, ambayo tayari imesababisha machafuko katika jimbo hilo la China linalojitawala na kusababisha Marekani kuanzisha mchakato wa vikwazo ya nchi hiyo ya Asia, shirika la AFP limeandika.

Kulingana na muswada wa pendekezo hilo uliochapishwa wiki iliyopita, sheria hiyo itaruhusu idara za usalama la China Bara kufanya shughuli zake kwa uwazi katika jiji la Hong Kong.

Wakati huo huo Marekani imebaini kwamba, "Hong Kong haiko tena chini ya mamlaka ya China".

Kwa upande wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, "Hong Kong haiko tena huru" na kwa hivyo inaweza kupoteza hali yake ya biashara.

Washington imeomba mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya muswada huo, lakini Beijing imefutilia mbali madai hayo ya Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.