Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI-USHIRIKIANO-UCHUMI

China yaahidi 'kujibu' dhidi ya hatua za Donald Trump

Rais Donald Trump na mwenzake wa China Xi Jinping wakati wa mazungumzo kuhusu mkataba wa biashara kati ya nchi hizo mbili. (picha ya kumbukumbu)
Rais Donald Trump na mwenzake wa China Xi Jinping wakati wa mazungumzo kuhusu mkataba wa biashara kati ya nchi hizo mbili. (picha ya kumbukumbu) BRENDAN SMIALOWSKI / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

China imeapa kuchukuwa hatua dhidi ya Marekani baada ya rais Donald Trump kutangaza kwamba anataka kuweka kikomo kwa raia wa China wanaoingia nchini Marekani na kuweka vikwazo vya kibiashara huko Hong Kong.

Matangazo ya kibiashara

Vita vya maneno vinaendelea kati ya Marekani na China, wakati huu janga la Corona linaendelea kuiathiri Marekani kwa kikubwa.

"Taarifa yoyote au hatua yoyote inayoathiri masilahi ya China itakabiliwa na hatua yetu ya ulipizaji kisasi," Zhao Lijian, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, amewaambia waandishi wa habari.

Hivi karibuni rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuweka vikwazo vipya dhidi ya China, akiituhumu tena kuhusika kwa maelfu ya vifo vilivyotokana na ugonjwa hatari wa Covid-19.

Alitangaza pia kutokubaliana na sheria ya usalama wa China kwa Hong Kong ambayo imeendelea kuzusha wasiwasi mkubwa katika jimbo hilo linalojitawala.

Rais Trump alisema kuwa China imekiuka makubaliano ya uhuru wa Hong Kong kwa kupitisha sheria ya usalama wa Kitaifa. Nakala ambayo inaruhusu kurudi kwa vyombo vya usalama vya China kwa koloni la zamani la Uingereza na ambayo kwa wengi ni tishio kwa uhuru wa eneo hilo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.