Pata taarifa kuu
JAPAN-CORONA-AFYA-UCHUMI

Japan kuanza kufungua mipaka yake kwa baadhi ya wasafiri

Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe akiondoa barakoa kabla ya mkutano na waandishi wa habari huko Tokyo Mei 25, 2020, wakati alitangaza kusitisha hali ya dharura nchini kote.
Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe akiondoa barakoa kabla ya mkutano na waandishi wa habari huko Tokyo Mei 25, 2020, wakati alitangaza kusitisha hali ya dharura nchini kote. KIM KYUNG-HOON / POOL / AFP

Japan inatarajia kurejesha hali ya kawaida katika sekta ya uchukuzi, hasa kufungua mipaka yake kwa wasafiri kutoka nchi zenye viwango vya chini vya maambukizi ya Corona, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linakuja wakati nchi hii imeanza kulegeza vizuizi ilivyoweka mapema mwaka huu ili kukabiliana na mgogoro wa kiafya, uliosababidshwa na janga la Corona.

Wakati mamlaka ilipiga marufuku raia wa kigeni kuingia nchini Japan Februari mwaka huu ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo hatari, wasafiri kutoka Thailand, Vietnam, Australia na New Zealand sasa wanaruhusiwa kusafiri kwenda Japan katika miezi ijayo.

Wizara ya Mambo ya nje ya Japan haijatoa maelezo zaidi kufikia sasa.

Shule, majumba ya sinema, kumbi za michezo na maduka makubwa yanafunguliwa tena Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Tokyo.

Japan imerekdi visa 17,000 vya maambukizi ya Corona, ugonjwa ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya watu karibu 900.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.