CHINA-HONG KONG-MAANDAMANO-USALAMA

Wakazi wa Hong Kong waendelea na maandamano mwaka mmoja baadaye

Waandamanaji lulaani ukandamizaji na mauaji yaliyotokea katika eneo la Tiananmen Square huko Beijing mwaka1989 huko Victoria Park, Hong Kong, Juni 4, 2020.
Waandamanaji lulaani ukandamizaji na mauaji yaliyotokea katika eneo la Tiananmen Square huko Beijing mwaka1989 huko Victoria Park, Hong Kong, Juni 4, 2020. REUTERS/Tyrone Siu

Wakazi wa Hong Kong wamerudi mitaani kwa mara nyinge mwaka mmoja baadaye kupinga utawala wa China kuingilia kati masuala ya ndani ya mji huo uliokuwa chini ya utawala wa Uingereza katika enzi za ukoloni.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka mmoja uliopita, Juni 9, 2019, watu zaidi ya milioni (240,000 kulingana na polisi) waliandamana dhidi ya "sheria ya kuwasafirisha washtumiwa nchini China", ambayo ingeliruhusu Beijing kumchukua na kumshughulikia mtu yeyote aliyekamatwa katika mji wa Hong Kong. Maandamano hayo yaliendelea,na kusitishwa lililpozuka janga la Corona mwezi Desemba mwaka jana.

Lakini leo na licha ya hatari ya kiafya, Beijing kwa mara nyingine imesababisha maandamano mengine makubwa ya wakazi wa Hong Kong kufuatia "sheria yake ya usalama wa taifa" wa Hong Kong.

Maandamano ya kwanza dhidi ya sheria ya ya kuwasafirisha washtumiwa nchini China, ilianza mwezi Machi 2019 na mkutano wa hadhara ulioitishwa na Chama kinachotetea demokrasia cha Demosisto (kilichoundwa baada ya "maandamano ya wanaharakati wanaotumia miamvuli" ya mwaka 2014) mbele ya majengo ya serikali.

Maandamano ya kukaa, yaliyoitwa Occupy Central, yalidai kuwa Beijing ijitoe kwenye mpango wake wa kuingilia uchaguzi wa mtawala wa juu kabisa wa Hong Kong, anayeitwa kiongozi mkuu, ambao ulimtaka yeyote anayegombea madaraka apate uungwaji mkono na walio wengi kutoka kwenye kamati ya uteuzi iliyojaa mashabiki wa Beijing (ambao ni watu wenye mrengo wa chama cha Kikomunisti cha China). Wakati huo maandamano ya kukaa yalienea kuanzia wilaya ya kiuchumi ya Admiralty mpaka wilaya ya kibiashara kwenye ghuba ya Causeway Bay na Mongkok. Idadi kubwa ya watu kwenye kisiwa cha Hong Kong iliendelea kuwepo mtaani siku nzima ya Septemba 29.

laki kwa wakati huu raia wa Hong Kongo wanapinga sheria ya usalama wa taifa wa Hong Kong , iliyopitishwa na Bunge la China.

Hata hivyo wakosoaji wa Beijing wanasema sheria itavuruga uhuru na hadhi ya mji wa Hong Kong.

China Bara imekuwa ikitumia mara kwa mara sheria ya kitaifa ya usalama kuwakamata wanaharakati, waandishi wa habari na wanasheria bila ya kuwafungulia mashitaka ama kuwapatia fursa ya kupata mawakili.