Bunge la Ulaya lataka Umoja wa Ulaya kuchukulia hatua kali China
Bunge la Ulaya limepitisha azimio kuomba Umoja wa Ulaya (EU) kuifungulia mashitaka China katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa huko Hague ikiwa Beijing itatoa sheria mpya ya usalama huko Hong Kong.
Imechapishwa:
Wabunge wa umoja wa Ulaya pia wametoa wito kwa viongozi wa umoja huo kuchukuwa vikwazo vya kiuchumi ili kuwashawishia viongozi wa China.
Bunge la Ulaya "limetoa wito kwa Umoja wa Ulaya na nchi wanachama kuchukuwa hatua ya kufungua mashitaka katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa, ikiwa sheria mpya ya usalama itatumika huko Hongo Kong, kumnyakua Korti ya Kimataifa ya Haki", imeandikwa kwenye azimio hilo.
Wabunge pia wameshauri viongozi wa Umoja wa Ulaya viongozi kuchukuwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya China.
Siku ya Jumatano wiki hii, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizostawi kiviwanda, G7, walitoa taarifa ya pamoja kuomba Beijing iachane na sheria hiyo mpya ya usalama wa kitaifa huko Hong Kong, ambayo wanasema inakiuka kanuni ya "nchi moja, mifumo miwili".
Muswada huo wa sheria unalenga kumaliza "uasi, maandamano, ugaidi na nchi za kigeni kuingilia kati" katika eneo hilo lililokuwa chini ya utawala wa kikoloni kutoka Uingereza, ambalo lilijiunga na China mnamo mwaka 1997.
Wakosoaji wa serikali ya Beijing wanaiona kama sheria hiyo ni tishio dhidi ya kanuni ya "nchi moja, mifumo miwili" ambayo inasimamia uhusiano kati ya utawala wa Beijing na "eneo maalum wa linalojitawala" tangu Hong Kong iliporudi chini ya utawala wa China na ambayo inapaswa kuhakikisha eneo hilo linakuwa ni uhuru na kuwa na jukumu lale kama kituo cha fedha cha kimataifa.