Urusi kusherehekea ushindi wa mwaka 1945, kabla ya kura ya maoni licha ya Covid-19
Imechapishwa:
Maelfu ya wanajeshi watafanya gwaride kwenye eneo la Red Square Jumatano wiki hi mbele ya Vladimir Putin, kama kukomaza uzalendo licha ya janga la Covid-19, kabla ya kura ya maoni inayolenga kuimarisha utawala wake.
Gwaride hili la kijeshi litakaloadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya ushindi dhidi ya utawala wa Kinazi; sherehe ambazo hapo awali zilipangwa kufanyika Mei 9, kama ilivyokuwa kila mwaka, lakini Kremlin ililazimika kuahirisha kwa sababu ya kusambaa kwa ugonjwa hatari wa Corona.
Ingawa Urusi bado ina maelfu ya kesi mpya za kila siku na kwamba Moscow, licha ya kulegeza masharti, inaendelea kupiga marufuku mikusanyiko ya umma.
Bwana Putin ametaka kuandaa gwaride hili Juni 24, tarehe iliyochaguliwa kuwa ya gwaride la kwanza la aina yake mnamo mwaka 1945.
Na tukio hili litafanyika, wiki moja tu kabla ya kura ya maoni itakayomuwezesha kuendelea kusalia madarakani hadi mwaka 2036.
Vladimir Putin pia amesifia hali ya utulivu inayojiri katika nchi ambayo ameitawala kwa miaka 20.
Urusi ni nchi ya tatu kuathiriwa zaidi na ugonjwa wa Covid-19 kwa maambukizi, ambapo visa 584,680 vya maambukizi na vifo 8,111 vilithibitishwa siku y Jumapili.
Hata hivyo miji kumi na tano imeamua kufuta gwaride la kijeshi.Katika mitaa ya Moscow, karibu askari 13,000 wa Urusi na wale kutoka nchi zingine kumi na tatu, ikiwa ni pamoja na India an China watashiriki gwaride hilo.