URUSI-USALAMA-CORONA-AFYA

Urusi yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 toka ipate ushindi dhidi ya Wanazi

Vladimir Putin na afisa ngazi ya juu wa mwisho wa cheo cha Marshal wa Dola ya Umoja wa Nchi za Kisovieti na Waziri wa zamani wa Ulinzi, Dmitry Iazov, Novemba 2014.
Vladimir Putin na afisa ngazi ya juu wa mwisho wa cheo cha Marshal wa Dola ya Umoja wa Nchi za Kisovieti na Waziri wa zamani wa Ulinzi, Dmitry Iazov, Novemba 2014. Alexey DRUZHININ / SPUTNIK / AFP

Urusi  leo inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya kumalizika kwa vita vya vya pili vya dunia, huku taifa hilo likitazamiwa kupiga kura ya maoni kumruhusu rais Vladmir Putin kuendelea kusalia madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajia kuhudhuria gwaride la kijeshi Jumatano wiki hii, siku moja kabla ya kura ya maoni ambayo inaweza kumuwezesha kusalia madarakani hadi mwaka 2036.

Gwaride hilo, ambalo lilitarajiwa kufanyika Mei 9 kwa maadhimisho ya miaka 75 ya ushindi wa Dola ya Umoja wa Nchi za Kisovieti (Urusi) dhidi ya utawala wa Kinazi, lilisogezwa mbele kwa sababu ya janga la Corona. Baadhi wanabaini kwamba kufanyika kwa maadhimisho hayo katika mazingira ya kiafya ya sasa ni kuiweka nchi hatarini.

Wakati wa uzinduzi wa kanisa kuu lililojengwa kwa heshima ya jeshi la Urusi, Putin alisema siku ya Jumatatu kwamba ushindi wa mwaka 1945 bado ni kumbukumbu takatifu kwa Urusi na jiwe kuu la historia yake.

Kura ya maoni, ambayo itafanyika kuanzia Juni 25 hadi Julai 1, inahusu marekebisho ya katiba ambayo yatamuwezesha Putin kusalia mamlakani kwa mihula mingine zaidi ya miaka sita.

Kama ilivyo, katiba ya sasa inamzuia kuwania tena wakati muhula wake utakapomalizika mnamo mwaka 2024.

Kulingana na taasisi ya kutabiri matokeo ya kura, VTsIOM, kura ya "ndio" itashinda kwa 71% dhidi ya 67%.

Zaidi ya askari 14,000 watashiriki katika gwaride hilo, ikiwa ni pamoja na magari 200 ya kivita na ndege 75.