INDIA-CORONA-AFYA

Idadi ya maambukizi ya Corona yapindukia zaidi ya nusu Milioni India

Karibu asilimia 90 ya wilaya masikini nchini India zina kesi za maambukizi, licha ya kuwa maambukizi zaidi yanabakia kuwa Delhi, Maharashtra, na Tamil Nadu, majimbo ambayo yana miji mikubwa.
Karibu asilimia 90 ya wilaya masikini nchini India zina kesi za maambukizi, licha ya kuwa maambukizi zaidi yanabakia kuwa Delhi, Maharashtra, na Tamil Nadu, majimbo ambayo yana miji mikubwa. XAVIER GALIANA / AFP

India imerekodi visa zaidi ya 500,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona, serikali imetangaza leo Jumamosi Juni 27, baada ya visa vipya 18,500 kuthibitishwa katika muda wa siku moja.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo ina jumla ya vifo 15,685 kwa sababu ya Covid-19, na kulingana na wanakolojia ugonjwa huu bado haujafikia kilele chake, kinachotarajiwa katika wiki kadhaa zijazo, na labda idadi ya wagonjwa inaweza kufikia milioni au zaidi ifikapo mwezi Julai, shirika la habari la AFP limeandika.

Wagonjwa 296 wamethibitishwa kupona ugonjwa huo hatari.

Baada ya kulegeza hatua za kuwazuwia watu kusalia majumbani mwao, serikali ya India imetumia treni maalum kuwarejesha maelfu ya wafanyakazi wahamiaji kwenda katika vijiji vyao katika wiki za hivi karibuni.

Karibu asilimia 90 ya wilaya masikini nchini India zina kesi za maambukizi, licha ya kuwa maambukizi zaidi yanabakia kuwa Delhi, Maharashtra, na Tamil Nadu, majimbo ambayo yana miji mikubwa.

Hayo yanajiri wakati mataifa mengi ya Ulaya yanafurhia ulegezwaji wa taratibu za kuwazuwia watu kusalia majumbani mwao lakini katika mahospitali mataifa hayo yanajitayarisha kwa wimbi la pili la maambukizi.