MAREKANI-CHINA-USHIRIKIANO

Washington yaimarisha shinikizo kwa Beijing kwa kutetea uhuru wa Hong Kong

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo hakuelezea idadi au maafisa hao wanaolengwa, lakini amebaini kwamba familia zao pia zinahusika.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo hakuelezea idadi au maafisa hao wanaolengwa, lakini amebaini kwamba familia zao pia zinahusika. Andrew Harnik/Pool via REUTERS

Washington imeongezea shinikizo kwa Beijing ili "kuwaadhibu" wale "wanaohusika" na kuivamia Hong Kong kwa kuwazuia kuingia nchini Marekani, wakati Bunge la Marekani linazimia kuchukuwa vikwazo zaidi.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump 'ameahidi kuwaadhibu maafisa wa Chama cha Kikomunisti nchini China ambao wamehusika kwa kuvunja uhuru wa Hong Kong," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amesema.

Ili kufanya hivyo, ametangaza 'kuwanyima visa' wajumbe wenye ushawishi mkubwa katika chama tawala nchini China ambao "wamehusika, au wamekula njama, kwa kuhatarisha uhuru wa Hong Kong" kama inavyoelezwa katika ahadi za kimataifa za Beijing.

Hatua hizi pia zinalenga wale waliohusika na "katika ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi" katika koloni hilo la zamani la Uingereza.

Mike Pompeo hakuelezea idadi au maafisa hao wanaolengwa, lakini amebaini kwamba familia zao pia zinahusika.

"Marekani inataka China kuheshimu ahadi zake,"ameaongeza waziri wa mambo ya nje wa Marekani, akitishia kuchukua hatua zaidi.

"Tunawasihi Wamarekani kukosoa makosa yao mara moja, kuondoa hatua hizi na kuacha kuingilia maswala ya ndani ya China," amesema Balozi wa China nchini MMarekani.

"China itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha uhuru wa kitaifa, usalama na maendeleo ya masilahi yake," ameongeza katika taarifa.

China ilitangaza mwezi uliopita muswada wenye utata wa kurudisha udhibiti wa usalama katika jimbo la Hong Kong, kauli ambayo ilikosolewa na upinzani nchini China na kwa sehemu kubwa jamii ya kimataifa kama njia ya kunyamanzisha wanaharakati wanaotetea demokrasia huko Hong Kong.