CHINA-HONG KONG-MAREKANI-USALAMA

China kuchukuwa vikwazo dhidi ya baadhi ya maafisa wa Marekani

Hivi karibuni China iliapa kuchukuwa hatua dhidi ya Marekani baada ya rais Donald Trump kutangaza kwamba anataka kuweka kikomo kwa raia wa China wanaoingia nchini Marekani na kuweka vikwazo vya kibiashara huko Hong Kong.
Hivi karibuni China iliapa kuchukuwa hatua dhidi ya Marekani baada ya rais Donald Trump kutangaza kwamba anataka kuweka kikomo kwa raia wa China wanaoingia nchini Marekani na kuweka vikwazo vya kibiashara huko Hong Kong. Greg Baker / AFP

Serikali ya China imebaini kwamba inataka kuchukuwa vikwazo vya kuwanyima visa baadhi ya maafisa wa Marekani baada ya uamuzi kama huo uliochukuliwa na Washington dhidi ya maafisa kadhaa wa Chama cha Kikomunisti cha China, na hii, ni kutokana na hatua ya Beijing kwa Hong Kong.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Zhao Lijian, katika mkutano na waandishi wa habari leo Jumatatu.

Hivi karibuni China iliapa kuchukuwa hatua dhidi ya Marekani baada ya rais Donald Trump kutangaza kwamba anataka kuweka kikomo kwa raia wa China wanaoingia nchini Marekani na kuweka vikwazo vya kibiashara huko Hong Kong.

Kauli hiyo ilikuja baada ya Washington kuongezea shinikizo kwa Beijing ili "kuwaadhibu" wale "wanaohusika" na kuivamia Hong Kong kwa kuwazuia kuingia nchini Marekani, wakati Bunge la Marekani linatazimia kuchukuwa vikwazo zaidi.

Rais wa Marekani Donald Trump 'aliahidi kuwaadhibu maafisa wa Chama cha Kikomunisti nchini China ambao wamehusika kwa kuvunja uhuru wa Hong Kong," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alisema.

Ili kufanya hivyo, ametangaza 'kuwanyima visa' wajumbe wenye ushawishi mkubwa katika chama tawala nchini China ambao "wamehusika, au wamekula njama, kwa kuhatarisha uhuru wa Hong Kong" kama inavyoelezwa katika ahadi za kimataifa za Beijing, Bw. Pompeo aliongeza.

China ilitangaza mwezi uliopita muswada wenye utata wa kurudisha udhibiti wa usalama katika jimbo la Hong Kong, kauli ambayo ilikosolewa na upinzani nchini China na kwa sehemu kubwa jamii ya kimataifa kama njia ya kunyamanzisha wanaharakati wanaotetea demokrasia huko Hong Kong.