CHINA-HONG KONG-USALAMA

Hong Kong: Chama cha Demosisto chavunjika kwa hofu juu ya sheria ya usalama

Bunge la China limepitisha sheria tata ya usalama ya kitaifa huko Hong Kong, vyombo vya habari katika eneo hilo linalojitawala vimebaini, na kuongeza hofu ya kukandamizwa kwa upinzani wa kisiasa katika koloni hilo la zamani la Uingereza.
Bunge la China limepitisha sheria tata ya usalama ya kitaifa huko Hong Kong, vyombo vya habari katika eneo hilo linalojitawala vimebaini, na kuongeza hofu ya kukandamizwa kwa upinzani wa kisiasa katika koloni hilo la zamani la Uingereza. REUTERS/Tyrone Siu

Chama cha siasa cha Demosisto huko Hong Kong, kilichoanzishwa na wanaharakati wanaotetea demokrasia, kimetangaza Jumanne hii alasiri, Juni 30, kuwa kimevunjika baada ya Bunge la China kupitisha sheria tata ya usalama wa kitaifa katika eneo hilo linalojitawala.

Matangazo ya kibiashara

"Baada ya kufikiria sana kwa undani, tumeamua kukivunja chama na kusitisha shughuli zote kama kundi kulingana na mazingira yaliopo sasa," chama cha Demosisto kimebaini kawenye ukurasa wake wa Twitter.

Bunge la China limepitisha sheria tata ya usalama ya kitaifa huko Hong Kong, vyombo vya habari katika eneo hilo, na kuongeza hofu ya kukandamizwa kwa upinzani wa kisiasa katika koloni hilo la zamani la Uingereza.

Hatua hiyo inatarajiwa kuchochea ghasia katika kitovu hicho cha kibiashara na kuongeza mvutano kati ya China na Marekani.

Hivi rais wa Marekani alitangaza kutokubaliana na sheria ya usalama wa China kwa Hong Kong ambayo imeendelea kuzusha wasiwasi mkubwa katika jimbo hilo linalojitawala.

Rais Trump alisema kuwa China imekiuka makubaliano ya uhuru wa Hong Kong kwa kupitisha sheria ya usalama wa Kitaifa.

Jumatatu wiki hii serikali ya China ilibaini kwamba inataka kuchukuwa vikwazo vya kuwanyima visa baadhi ya maafisa wa Marekani baada ya uamuzi kama huo uliochukuliwa na Washington dhidi ya maafisa kadhaa wa Chama cha Kikomunisti cha China, na hii, ni kutokana na hatua ya Beijing kwa Hong Kong.

Kauli hiyo ilitolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Zhao Lijian, katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu Juni 29.

Sheria hiyo itawaadhibu wanaojihusisha na kutaka kujitenga, kudhoofisha nguvu ya serikali, ugaidi na vitendo vyote vinavyotishia usalama wa taifa.