CHINA-HONG KONG-USALAMA

Polisi ya Hong Kong yasambaratisha waandamanaji, watu kadhaa wakamatwa

Vikosi vya usalama pia vimezingira watu wengi kwenye mitaa ya eneo la kibiashara katika mji wa Hong Kong na wengine wamepelekwa karibu na jengo la jengo la bunge katika eneo hilo.
Vikosi vya usalama pia vimezingira watu wengi kwenye mitaa ya eneo la kibiashara katika mji wa Hong Kong na wengine wamepelekwa karibu na jengo la jengo la bunge katika eneo hilo. REUTERS

Polisi ya Hong Kong imetawanya makundi madogo ya waandamanaji Jumatano Julai 1 kwa kutumia maji licha ya maaandamano hayo kupigwa marufuku kufuatia sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyopitishwa Jumanne wiki hii na Bunge la China, shirika la habari la AFP limebaini.

Matangazo ya kibiashara

Polisi imetangaza kwamba imewakamata baadhi ya watu waliokuwa miongoni mwa waandamanaji na watakabiliwa na adhabu kali kulingana na sheria mpya ya usalama iliyopitishwa siku ya Jumanne.

Mtu aliyepatikana na bendera ya uhuru ya Hong Kong ndiye mtu wa kwanza kukamatwa chini ya sheria mpya ya usalama wa kitaifa, polisi imesema.

"Mtu mmoja amekamatwa akiwa na bendera ya uhuru ya Hong Kong huko Causeway Bay, na hii ni ukiukaji wa sheria za usalama wa nchi," polisi imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, huku ikibaini kwamba huu ni mtu wa kwanza kukamatwa tangu kuanza kutumia sheria mpya ya usalama.

Hata hivyo vyanzo kadhaa kutoka Hong Kong vimebaini kwamba watu zaidi ya thelathini wamekamatwa.

Marekani kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje Mike Pompeo ameitishia serikali ya Beijing kwa kuchukulia hatua kali baada ya kupitishwa sheria hiyo mpya kuhusu usalama wa kitaifa.

Hivi karibuni Rais wa Marekani Donald Trump alisema kuwa China imekiuka makubaliano ya uhuru wa Hong Kong kwa kupitisha sheria ya usalama wa kitaifa. Nakala ambayo inaruhusu kurudi kwa vyombo vya usalama vya China kwa koloni la zamani la Uingereza na ambayo kwa wengi ni tishio kwa uhuru wa eneo hilo.

Sheria hiyo itawaadhibu wanaojihusisha na kutaka kujitenga, kudhoofisha nguvu ya serikali, ugaidi na vitendo vyote vinavyotishia usalama wa taifa.