BURMA-MAJANGA YA ASILI

Burma: Maporomoko ya udongo yaua watu zaidi ya 100 katika mgodi wa Jade

Waokoaji wanajaribu kupata manusura baada ya maporomoko ya udongo katika mgodi wa Jade wa Hpakant, katika Jimbo la Kachin nchini Burma, Julai 2, 2020.
Waokoaji wanajaribu kupata manusura baada ya maporomoko ya udongo katika mgodi wa Jade wa Hpakant, katika Jimbo la Kachin nchini Burma, Julai 2, 2020. Handout / MYANMAR FIRE SERVICES DEPARTMENT / AFP

Watu 113 wamepoteza maisha katika kisa cha maporomoko ya udongo katika mgodi wa Jade, Kaskazini mwa Burma. Kulingana na vyanzo vya usalama wachimba migodi wamesombwa na matope yaliyosababishwa na mafuriko.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Burma inasema kuwa zoezi la uokoaji linaendelea

Hii ni idadi kubwa ya vifo kutokea nchini Burma kufuatia majanga ya asili.

Miili 1130ya watu waliofariki dunia iliondolewa katikia matope, na zoezi la kutafuta miili na watu waliohai limesitishwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

"Kufikia sasa tumepata jumla ya miili 113," idara ya Zima Moto imeandika kwenye ukurasa wake wa Facebook. Kwenye ukurasa huu, picha zinaonyesha timu ya waokoaji wakipanda kwenye mlima uliojaa matope, kwenye korongo la Hpakant, karibu na mpaka wa China.

Kila mwaka, makumi kadhaa ya wachimba migodi wanaotafuta mawe ya thamani hufariki dunia katika ajali zinazosababishwa na mazingira magumu ya kazi, hasa wakati wa msimu wa mvua.