MAREKANI-CHINA-HONG KONG-USALAMA

Marekani kuichukulia vikwazo zaidi China

Jumanne wiki hii Bunge la China lilipitisha sheria tata ya usalama ya kitaifa huko Hong Kong.
Jumanne wiki hii Bunge la China lilipitisha sheria tata ya usalama ya kitaifa huko Hong Kong. DALE DE LA REY / AFP

Wabunge nchini Marekani wamepitisha muswada wa vikwazo dhidi ya uongozi wa China baada kupitishwa kwa sheria tata ya usalama inayoonekana kuminya uhuru wa watu wanaoishi katika eneo la Hong Kong.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni kwa vikwazo hivyo ni kuzuia biashara za Benki zinazoshirikiana na maafisa wa China.

Muswada huo sasa unatarajiwa kupelekwa katika Bunge la Senate kabla ya kutiwa saini na rais Donald Trump.

Sheria hizo mpya za usalama zimelaaniwa na Uigereza, mkoloni wa zamani wa Hong Kong, kabla ya kukabidhi mji huo kwa China mwaka 1997.

Jumanne wiki hii Bunge la China lilipitisha sheria tata ya usalama ya kitaifa huko Hong Kong, na kuongeza hofu ya kukandamizwa kwa upinzani wa kisiasa katika koloni hilo la zamani la Uingereza.

Hivi karibuni Rais Trump alisema kuwa China imekiuka makubaliano ya uhuru wa Hong Kong kwa kupitisha sheria ya usalama wa Kitaifa. Nakala ambayo inaruhusu kurudi kwa vyombo vya usalama vya China kwa koloni la zamani la Uingereza na ambayo kwa wengi ni tishio kwa uhuru wa eneo hilo.

Jumatatu wiki hii serikali ya China ilibaini kwamba inataka kuchukuwa vikwazo vya kuwanyima visa baadhi ya maafisa wa Marekani baada ya uamuzi kama huo uliochukuliwa na Washington dhidi ya maafisa kadhaa wa Chama cha Kikomunisti cha China, na hii, ni kutokana na hatua ya Beijing kwa Hong Kong.