INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: India yarekodi visa 700,000 vya maambukizi

Watu wakivaa barakoa wakijilinda dhidi ya maambukizi ya corona kwenye kituo cha mabasi huko Kochi, katika Jimbo la Kerala, India.
Watu wakivaa barakoa wakijilinda dhidi ya maambukizi ya corona kwenye kituo cha mabasi huko Kochi, katika Jimbo la Kerala, India. AP Photo/R S Iyer

India imekuwa nchi ya tatu kwa idadi kubwa ya maambukizi ya visa vya maambukizi, baada ya Marekani na Brazili, baada ya kurekodi visa 700,000 vya maambukizi, kulingana na takwimu zilizotolewa na mamlaka leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo, yenye wakazi zaidi ya bilioni 1.3, ambayo inazidi Urusi kwa idadi ya maambukizi, inachukuwa nafasi ya tatu duniani kwa maambukizi baada ya Brazil.

Wizara ya Afya ya India imetangaza leo Jumatatu kuwa zaidi ya kesi 23,000 zimerekodiwa katika muda wa saa 24

Kesi 25,000 za maambukizi zilithibitishwa Jumapili Julai 5.

Karibu watu 14,000 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19 nchini India tangu kupatikana kwa mtu wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya SARS-CoV-2 mwezi Januari.

India imerekodi kesi za maambukizi mara nane zaidi kuliko China, ambayo ina wakazi sawa nchi hiyo; ambapo ulianzia ugonjwa huo mwishoni mwa mwaka jana.

Mamlaka imefuta hatua ya kufungua tena Taj Mahal, kivutio maarufu zaidi cha utalii, katika mji wa Agra, kilomita 200 kutoka mji wa New Delhi, baada ya mlipuko mpya wa maambukizi ya virusi vya Corona katika jimbo hilo.