CHINA-CORONA-USALAMA-HAKI

China yafungulia mashitaka watu 23 waliosababisha maafa makubwa katika hoteli ya Xinjia

Shughuli za uokoaji katika baada ya hoteli ya Xinjia iliyokuwa inatumiwa katika kuwapokea watu wanaowekwa karantini, kuporomoka, huko Quanzhou, mashariki mwa China, Machi 7, 2020.
Shughuli za uokoaji katika baada ya hoteli ya Xinjia iliyokuwa inatumiwa katika kuwapokea watu wanaowekwa karantini, kuporomoka, huko Quanzhou, mashariki mwa China, Machi 7, 2020. AFP

Mamlaka nchini China imewashtaki watu 23 kwa kufanya mabadiliko haramu ya ujenzi wa hoteli moja iliyokuwa ikitumiwa kwa kuwapokea watu wanaoshukiwa kuwa na dadlili za ugonjwa wa Covid-19, baada ya jengo hilo kuporomoka na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Watu 29 walipoteza maisha na wengine 42 kujeruhiwa katika tukio hilo lililotokea mwezi Machi mwaka huu, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti leo Jumanne.

Hoteli ya Xinjia, jengo la vyumba 66 iliyopo katika mji wa pwani wa Quanzhou katika mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China, liliporomoka mnamo Machi 7, na kusababisha kukwama watu kadhaa waliyokuwa waliwekwa karantini baada ya kusafiri katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ugonjwa wa Corona.

Uchunguzi rasmi uligundua kuwa ghorofa tatu ziliongezwa kinyume cha sheria kwa muundo wa awali wa ghorofa nne na kwamba maafisa wa usalama wakishirikiana na mmiliki wa jengo hoteli hiyo, waliwasilisha ripoti za uwongo hukusu jengo hilo, runinga ya CCTV imeripoti.

"Hatua kali" zimechukuliwa dhidi ya watu 23 waliohusika katika kazi hiyo na maafisa wa eneo hilo wanachunguzwa kwa madai ya ufisadi kuhusiana na kuporomoka kwa jengo hilo, kulingana na runinga ya CCTV.

Meya wa mji wa Quanzhou, Wang Yongli, ameshtumiwa kwa kutowajibika kwa majukumu yake, na pia maafisa wengine kadhaa, maafisa wa kitengo cha kupambana na ufisadi katika mkoa wa Fujian wamesema katika taarifa.

Ukarabati wa ghorofa ya kwanza ya hoteli hiyo ulikuwa unaendelea na ulianza kabla ya Mwaka mpya wa jadi wa kichina, ambao ulianza Januari 25 mwaka huu.

Wafanyikazi waliripoti kwa mmiliki wa hoteli hiyo kuhusu kasoro kwenye moja ya nguzo zinlizokuwa zinashikilia jengo hilo, muda mfupi kabla ya jengo hilo kuporomoka, Wizara yenye dhamana ya Hali ya Dharura imesema.

Watu wote waliokuwa wamliwekwa karantini katika hoteli hiyo walipimwa na kukutwa hawana maambukizi ya Covid-19, kulingana na Gazeti la kila siku la Quanzhou Evening News.