ARMENIA-AZERBAIJAN-USALAMA

Mapigano yarindima kwenye mpaka wa kati ya Armenia na Azerbaijan

Mapigano kati ya nchi mbili jirani, Armenia na Azerbaijan yameanza tena leo Alhamisi asubuhi kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili, baada ya saa 24 mapigano hayo kusitishwa.

Wanajeshi wa Armenia wakibeba matairi yaliyotumiwa nyuma ya lori kuimarisha ngome zao kwenye mpaka na Azerbaijan, Julai 15, 2020.
Wanajeshi wa Armenia wakibeba matairi yaliyotumiwa nyuma ya lori kuimarisha ngome zao kwenye mpaka na Azerbaijan, Julai 15, 2020. Karen MINASYAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo imeendelea kuzua wasiwasi mkubwa katika nchi hizo jirani.

Hata hivyo usitishwaji mapigano haukudumu muda mrefu. Milio ra risasi na milipuko vimeendelea kusikita tangu mapema asubuhi kwenye mpaka wa Kaskazini unao ambao unazigawa nchi hizo mbili.

Kila upande umemtuhumu mwenzake kwa kufanya mashambulizi dhidi ya ngome za kijeshi za mwingine pamoja na vijiji.

Wanajeshi zaidi ya 10 wa Azerbaijan na raia mmoja pamoja na wanajeshi wanne wa Armenia wameuwawa tangu siku ya Jumapili katika mgogoro uliozuka upya kati ya nchi hizo zilizokuwa jamhuri za kisovieti.

Nchi hizi mbili ziliwahi kupigana katika miaka ya 1990 kwenye vita vya milimani katika jimbo la Nagorno Karabakh.

Jumuiya ya kimataifa imesema ina wasiwasi kutokana na kuwa mapigano hayo mapya yanatishia hali ya uthabiti wa eneo hilo ambalo linatumiwa kama njia ya mabomba yanayosafirisha mafuta na gesi kutoka Bahari ya Caspian hadi kwenye masoko ya ulimwengu.