CHINA-MAREKANI-USHIRIKIANO

China yatakiwa kufunga ubalozi wake mdogo Houston, nchini Marekani

Marekani imeitaka China kufunga ubalozi wake mdogo katika jiji la Texas katika Jimbo la Houston, Wizara ya Mambo ya nje ya China imesema leo Jumatano, ikilaani vikali uamuzi huo na kutishia kuchukua hatua za kulipiza kisasi.

Mvutano kati ya Marekani na China unaendelea.
Mvutano kati ya Marekani na China unaendelea. REUTERS/Aly Song
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kila siku, msemaji wa wizara ya mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin, amesema Beijing iliarifiwa ghafla kuhusu hatua hiyo Jumanne wiki hii. Hata hivyo hakutoa sababu za Marekani kuitaka China kufunga ubalozi wake mdogo huko Texas.

Mamlaka nchini Marekani imeipa China siku tatu kuwa imefunga ubalozi wake mgodo Texas, Wang Wenbin amesema.

"Hatua ya Marekani kufunga ubalozi wa China huko Houston, bila hata hivyo kuishirikisha serikali ya Beijing, katika kipindi kifupi kama hiki ni muendelezo wa hatua za hivi karibuni za Marekani dhidi ya China," Wenbin ameongeza.

"Tunaiomba Marekani kurejelea uamuzi huo mbaya mara moja. Kama itaendelea kushikilia uamzi wake huo mbaya, China italipiza kisasi kwa kuchukuwa hatua kali, " amebaini msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China."

Pia amehakikisha kwamba ubalozi huo ulikuwa unaendesha shughuli zake za kawaida, bila hata hivyo kutoa maoni yake juu ya habari kutoka vyombo vya habari vya Texas ambazo zinadai kuwa kuna hati ambazo zilichomwa moto jana Jumanne jioni katika eneo la jengo hilo.

"Inaonekana kama kuna vitu vilivyochomwa moto katika kontena kwenye eneo la jengo la ubalozi. Lakini hatukuruhusiwa kuingia," mkuu wa idara ya Zima Moto wa Jimbo la Houston amesema kwenye kituo cha habari cha KTRK.

Akiwa ziarani jijini London Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, alitoa wito Jumanne kwa kuunda muungano wa kimataifa ili kuzuia "tishio" alilodai kutoka China.