URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Karibu kesi mpya 6,000 za maambukizi zahtibitishwa Urusi

Mamlaka ya afya nchini Urusi imeripoti visa vipya 5,862 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa 24 zilizopita, wakati idadi ya maambukizi ikiendelea kuongezeka duniani.

Ugonjwa aw Covid-19 unaendelea kuiathiri Urusi, ambayo ni ya nne kwa maambukizi duniani.
Ugonjwa aw Covid-19 unaendelea kuiathiri Urusi, ambayo ni ya nne kwa maambukizi duniani. REUTERS/Tatyana Makeyeva
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa na watu 789,190 walioambukizwa virusi vya Corona kwa jumla, Urusi ni nchi ya nne duniani ambayo imeathiriwa zaidi na virusi kwa idadi kubwa ya maambukizi.

Urusi pia imerekodi vifo vipya 165 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Idadi ya vifo vinavyotokana na janga hilo sasa imepindukia 12,745. Wagonjwa 572,000 wamepona ugonjwa huo hatari.

Hayo yanajiri wakati Shirika la Afya Duniani linaonya kuwa janga la Covid-19 linaendelea kuwa baya zaidi ulimwenguni na kwamba huenda hali ya kawaida iliyokuwepo zamani isirejee hivi karibuni.

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona imepindukia watu Milioni 15 duniani baada ya watu laki 2na Elfu 14 kuambukizwa katika muda wa saa 24 zilizopita, na zaidi ya watu 617,000 wamefariki, huku Marekani ikiendelea kurekodi idadi ya juu ya maambukizi mapya.

Hivi karibuni Mkuu wa shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus aliezitaka nchi kuweka mkakati kabambe wa kukabili idadi inayozidi kuongezeka ya maambukizi mapya, huku akisema kuwa nusu ya jumla ya maambukizi mapya hutokea mataifa ya Amerika.

Naye Dkt Mike Ryan, Mkurugenzi wa dharura katika shirika la Afya Duniani, alisema kuwa kulegeza masharti ya kutotoka nje katika nchi za Amerika na kufungua baadhi ya maeneo kumesababisha maambukizi kuongezeka kwa kiasi kikubwa''.