URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yapindukia zaidi ya 820,000 Urusi

Urusi imerekodi visa vipya 5,395 za maambukizi ya Corona leo Jumanne, na kufanya jumla ya idadi ya visa vya maambukizi kufikia 823,515 nchini humo.

dadi ya vifo imeongezeka kwa visa vipya 150 katika muda wa saa 24 zilizopita na kufanya jumla ya watu waliofariki dunia kufikia 13,504 nchini Urusi tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo.
dadi ya vifo imeongezeka kwa visa vipya 150 katika muda wa saa 24 zilizopita na kufanya jumla ya watu waliofariki dunia kufikia 13,504 nchini Urusi tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo. REUTERS/Tatyana Makeyeva
Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa Urusi inachukuwa nafasi ya nne duniani kwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Idadi ya vifo imeongezeka kwa visa vipya 150 katika muda wa saa 24 zilizopita na kufanya jumla ya watu waliofariki dunia kufikia 13,504 nchini tangu kuzuka kwa janga hilo.

Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kuwa hatua ya kufunga mipaka ya kimataifa sio suluhu kwa kudhibiti ugonjwa hatari wa Covid-19, bali itazidisha hali kuwa mbaya zaidi.

Kauli hiyo ya WHO inakuja wakati serikali kadhaa duniani zimechukua hatua za kurejesha vizuizi vya kukabiliana na janga la virusi vya corona zikijaribu kuepuka wimbi jipya la maambukizi wakati idadi ya vifo vilivyotokana na COVID-19 imepindukia 650,000.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuhusu kuendelea kufunga mipaka ya kimataifa likibaini kwamba itakuwa italeta shida zaidi, na kuongeza kuwa hiyo siyo njia shahihi ya kukambana na maambukizi zaidi ya Covid-19.