MALAYSIA-HAKI

Kashfa ya ufisadi ya 1MDB: Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib Razak apatikana na hatia

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib Razak alipofika katika mahakama ya Duta kusikiliza uamuzi wa kwanza katika kesi ya 1MDB, Kuala Lumpur Julai 28, 2020.
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib Razak alipofika katika mahakama ya Duta kusikiliza uamuzi wa kwanza katika kesi ya 1MDB, Kuala Lumpur Julai 28, 2020. Mohd RASFAN / AFP

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib Razak amepatikana na hatia Jumanne Julai 28 kwa makosa yote katika kesi yake ya kwanza ya kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya dola yaliyokuwa yametolewa na serikali kwa ajili ya mradi wa maendeleo.

Matangazo ya kibiashara

Fedha hizo zilikuwa ni pamoja na karibu dola milioni 700 ambazo wachunguzi wa Marekani wanasema ziliingia kwenye akaunti ya benki ya Najib. Wachunguzi hao wa Marekani wamesema washirika wa Najib waliiba kiasi cha dola bilioni 4.5 kutoka kwenye mfuko wa 1MDB alioanzisha kati ya mwaka 2009 na mwaka 2014, huku baadhi ya fedha hizo zikiwa zimeingizwa kwenye akaunti ya benki ya Najib.

"Baada ya kuchunguza ushahidi wote katika kesi hii, naona kwamba upande wa mashtaka umethibitisha kesi yake bila ya shaka yoyote," amesema Mohamad Nazlan Mohamad Ghazali, jaji katika Mahakama Kuu ya Kuala Lumpur.

Fedha hizo ziliibiwa na kuelekezwa katika matumizi binafsi, yakiwemo ununuzi wa magari ya anasa na kazi za sanaa zenye gharama kubwa.

Hata hivyo Bw. Razak mwenye umri wa miaka 67, amekanusha madai yote yanayomkabili katika kesi hiyo.

Haijafahamika iwapo Bw. Najib Razak atakataa rufaa au la.