KOREA KASKAZINI-CORONA-AFYA

Pyongyang yaimarisha hatua dhidi ya Covid-19 baada ya kesi ya kwanza ya maambukizi

Mamlaka nchini Korea Kaskazini imechukua uamuzi wa kumarisha hatua za kuzuia dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19 baada ya kutangazwa kesi ya kwanza ya maambukizi.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alitangaza hali ya dharura huko Kaesong, baada ya kugunduliwa kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona, ambaye alirejea nchini kinyume cha sheria Julai 19.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alitangaza hali ya dharura huko Kaesong, baada ya kugunduliwa kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona, ambaye alirejea nchini kinyume cha sheria Julai 19. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hatua kali za vizuizi na vipimo zinaendelea kujadiliwa, shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limesema. Vipimo, mavazi ya kinga na vifaa vya matibabu pia vimepelekwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Siku ya Jumapili, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alitangaza hali ya dharura huko Kaesong, baada ya kugunduliwa kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona, ambaye alirejea nchini kinyume cha sheria Julai 19.

Mji huo, unaopatikana kwenye mpaka na Korea Kusini, umezingirwa na vikosi vya usalama na wakazi wamepigwa marufuku kutotembea.

Pyongyang inasema ilifanya vipimo vya watu 1,211 kufikia Julai 16 na hakua mtu yeyote aliyepatikana na virusi vya Corona, kulingana na takwimu zilizotumwa kwa shirika la habari la Reuters na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Ripoti hii pia inabaini kuwa watu 700 kutoka Korea Kaskazini wamewekwa karantini.Tangu kuzuka kwa janga la Corona, Korea Kaskazini imepokea vifaa vingi vya kupima virusi vya ugonjwa huo hatari kutoka Urusi na nchi zingine.