URUSI-CORONA-AFYA

Karibu watu 8,000,000 waambukizwa virusi vya Corona Urusi

Urusi imerekodi kesi mpya 5,475 za maambukizi ya virusi vya Corona, na kufikisha jumla ya visa 828,990 vya maambukizi, na kuifanya kuwa nchi ya nne duniani kuathirika zaidi na ugonjwa huo hatari.

Kufikia sasa Urusi inachukuwa nafasi ya nne duniani kwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Kufikia sasa Urusi inachukuwa nafasi ya nne duniani kwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona. DIMITAR DILKOFF / AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo imeongezeka kwa visa vipya 169 katika muda wa saa 24 zilizopita na kufanya jumla ya watu waliofariki dunia kufikia 13,673 nchini tangu kuzuka kwa janga hilo.

Kufikia sasa Urusi inachukuwa nafasi ya nne duniani kwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Mapema wiki hii Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kuwa hatua ya kufunga mipaka ya kimataifa sio suluhu kwa kudhibiti ugonjwa hatari wa Covid-19, bali itazidisha hali kuwa mbaya zaidi.

Kauli hiyo ya WHO inakuja wakati serikali kadhaa duniani zimechukua hatua za kurejesha vizuizi vya kukabiliana na janga la virusi vya corona zikijaribu kuepuka wimbi jipya la maambukizi wakati idadi ya vifo vilivyotokana na COVID-19 imepindukia 650,000.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuhusu kuendelea kufunga mipaka ya kimataifa likibaini kwamba itakuwa italeta shida zaidi, na kuongeza kuwa hiyo siyo njia shahihi ya kukambana na maambukizi zaidi ya Covid-19.