HONG KONG-USALAMA-HAKI

Watu wanne wakamatwa chini ya sheria za usalama Hong Kong

China iliweka sheria hii mpya mwezi mmoja uliyopita, katika koloni la zamani la Uingereza ili kuadhibu kile inachokielezea kama ugaidi, kujitenga na kushirikiana na vikosi vya kigeni - kosa linaloadhibiwa na 'kifungo cha maisha.
China iliweka sheria hii mpya mwezi mmoja uliyopita, katika koloni la zamani la Uingereza ili kuadhibu kile inachokielezea kama ugaidi, kujitenga na kushirikiana na vikosi vya kigeni - kosa linaloadhibiwa na 'kifungo cha maisha. REUTERS

Polisi ya Hong Kong imetangaza kuwa imewakamata watu wanne, wenye umri wa miaka 16 hadi 21, kwa tuhuma za ukiukaji wa sheria mpya ya usalama wa kitaifa. Hii ni hatua ya kwanza ya kuwaweka watu kizuizini kwa madai yasiyohusiana na maandamano dhidi ya serikali tangu kupitishwa kwa sheria hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumatano jioni, msemaji wa polisi alisema wanaume watatu na mwanamke mmoja, ambao wote ni wanafunzi wote, walishukiwa kuwa sehemu ya kundi la watu wanaotoa taarifa mitandaoni kuhimiza wakazi wa eneo la Hon Kong kuwa watatumia njia zote zinazowezekana kwa kupigania uhuru wa Hong Kong.

China iliweka sheria hii mpya mwezi mmoja uliyopita, katika koloni la zamani la Uingereza ili kuadhibu kile inachokielezea kama ugaidi, kujitenga na kushirikiana na vikosi vya kigeni - kosa linaloadhibiwa na 'kifungo cha maisha.

Nchi kadhaa za Magharibi, viongozi wa makampuni makubwa na makundi ya wanaharakati walilaani sheria hiyo mpya wakisema kuwa ni hatua mpya ya Beijing inakuja kuimarisha udhibiti wake kwa Hong eneo nzima la Kong.

China inachukulia sheria hiyo kuwa muhimu kwa kuleta utulivu katika eneo hilo maalum la utawala baada ya maandamano yenye machafuko mwaka uliopita.