Coronavirus: Idadi ya maambukizi yapindukia 840,000 Urusi
Urusi imerekodi kesi mpya 5,482 za maambukizi ya virusi vya Corona leo Ijumaa, na kufanya jumla ya watu walioambukizwa virusi hivyo kufikia 839,981, idadi ambayo inaifanya nchi hiyo kuwa ya nne dunia iliyoathirika zaidi na ugnjwa huo.
Imechapishwa:
Mamlaka nchini humo inasema watu 161 wamefariki dunia katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufanya idadi ya vifo kufikia 13,963.
Hayo yanajiri wakati shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kwamba kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona katika nchi kadhaa kumesababishwa na vijana wapuuzi wasiojali kujikinga.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus amewatadharisha vijana kwamba wao pia wanawezwa kuambukizwa.
Mpaka sasa watu milioni 17 wamekumbwa na maambukizi hayo duniani kote na 670,000 wameshakufa. Bwana Tedros amesisitiza kuwa vijana pia wanaweza kufa kutokana na maradhi ya Covid 19 na pia wanaweza kuwaambukiza watu wengine.