JAPANI-HIROSHIMA-CORONA-AFYA

Japan yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya shambulizi la bomu la atomiki Hiroshima

Mtu huyo akisimama mbele ya Jumba la ukumbusho kwa waathiriwa shambulizi la bomu la atomiki huko Hiroshma kwenye Bustani ya Amani, Agosti 6, 2020.
Mtu huyo akisimama mbele ya Jumba la ukumbusho kwa waathiriwa shambulizi la bomu la atomiki huko Hiroshma kwenye Bustani ya Amani, Agosti 6, 2020. Philip FONG / AFP

Japan inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya shambulizi la bomu la atomiki katika historia yake. Bomu la pili la aina hiyo liliangushwa Nagasaki siku tatu baadaye.

Matangazo ya kibiashara

Imepita miaka 71 tangu Japan kukumbwa na maafa ya Hiroshima yaliyosababishwa na bomu la atomiki lililorushwa na Marekani tarehe 6 Agosti mwaka 1945 wakati wa vita vya pili vya dunia.

Shambulizi hilo la bomu la atomiki lililotekelezwa kwa mara ya kwanza duniani lilisababisha maafa makubwa na kuharibu miji iliyopakana na Hiroshima na kupelekea vifo vya watu 70,000.

Wajapan wameendelea kuwa na hofu kubwa kutokana na janga la Corona na kusababisha kusahau yaliyotokea katika miji wa Hiroshima na Nagasaki. Sherehe za kuwakumbuka wahanga wa tukio hilo huko Hiroshima zimefutwa. Virusi hivyo huzuia watoto wa shule za Japan kutoka kwa makundi kutembelea Bustani ya Amani, jumba lake la ukumbusho lililojengwa kwenye kitovu cha mlipuko wa bomu hilo la atomiki, 'jumba la kumbukumbu'.

Majira ya saa mbili na robo asubuhi ya tarehe 6 Agosti 1945, ndege ya kijeshi ya Marekani chapa B-29 Enola Gay iliangusha bomu lililopewa jina la "Mvulana Mdogo" na kuwauwa hapo hapo watu 140,000 kati ya wakaazi 350,000 wa mji huo.

Maelfu ya wengine walikufa siku za baadaye kutokana na majeraha na mionzi ya atomiki. Alkhamis ya leo, katika muda huo huo bomu hilo liliporipuka, watu walisimama na kunyamaza kimya kwa muda kuwakumbuka wahanga hao.

Waziri Mkuu Shinzo Abe alihudhuria kumbukumbu hiyo kama kawaida, lakini wageni kutoka jumuiya ya kimataifa walikuwa wachache.