BELARUS-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Belarus: Alexander Lukashenko athibitishwa kushinda uchaguzi wa urais

Svetlana Tikhanovskaya na Maria Kolesnikova, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii, Agosti 10. S. Tikhanovskaïa, kiongozi mkuu wa upinzani, amemuomba rais anayemaliza muda wake A. Loukachenko, aliyechaguliwa rasmi, "aondoke madarakani".
Svetlana Tikhanovskaya na Maria Kolesnikova, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii, Agosti 10. S. Tikhanovskaïa, kiongozi mkuu wa upinzani, amemuomba rais anayemaliza muda wake A. Loukachenko, aliyechaguliwa rasmi, "aondoke madarakani". Sergei GAPON / AFP

Shirika la habari la serikali ya Belarus limethibitisha ushindi wa rais anaymaliza muda wake Alexander Lukashenko aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi huo, kwa zaidi ya asilimia 80 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais jana Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Mshindani wake mkuu Svetlana Tikhanovskaïa, aliyepata 9.9% ya kura, amemuomba rais Alexander Lukashenko "kuondoka madarakani".

Kumekuwa kunatarajiwa maandamano mapya ya upinzani leo jioni.

Rais wa Belarus, ambaye yupo madarakani tangu mwaka 1994, amepata asilimia kubwa katika uchaguzi wa urais na hivyo kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika Jumapili Agosti 9. kulingana na takwimu za awali na ambazo ni rasmi zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi: Alexander Lukashenko ameshinda uchaguzi kwa asilimia 80.2 huku mshindani wake mkuu Svetlana Tikhanovskaïa akipata 9.9% ya kura, kwa mujibu wa mwandishi wetu huko Minsk, Daniel Vallot.

Mkuu wa tume ya uchaguzi, Lidia Yermoshina amesema kupitia televisheni kwamba mpinzani wa Lukashenko, mwanamama Svetlana Tikhanovskaya amepata asilimia 9.9 kulingana na matokeo ya awali. Hata hivyo, Tikhanovskaya amekataa kuyatambua matokeo hayo ya uchaguzi. Wagombea wengine watatu wameibuka na asilimia chini ya mbili kila mmoja. Tangazo hilo limetolewa baada ya polisi kuutawanya umati wa waandamanaji kwa kutumia mabomu na risasi za mpira katika mji mkuu wa Minsk na miji mingine Jumapili jioni.

Urusi imekaribisha matokeo hayo. wakati huo huo rais wa Urusi Vladimir Putin alituma "ujumbe wa kumpngeza rais wa Belarus Alexander Lukashenko, kulingana na Kremlin, na kuongeza: "Nina imani kuwa hatua yako kama mkuu wa nchi itawezesha maendeleo ya baadaye ya uhusiano kati ya Urusi na Belarus kuwa ni yenye manufaa makubwa.