BELARUS-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Belarus: Makabiliano yazuka Minsk baada ya Lukashenko kutangazwa mshindi wa uchaguzi

Vikosi vya usalama vimewatawanya waandamanaji wa upinzani baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa huko Minsk, Belarusi, Agosti 9, 2020.
Vikosi vya usalama vimewatawanya waandamanaji wa upinzani baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa huko Minsk, Belarusi, Agosti 9, 2020. Dmitry Brushko/Tut.By via REUTERS

Rais anayemaliza muda wake Alexander Lukashenko, ambaye yuko madarakani kwa miaka 26 nchini Belarus, amechaguliwa tena kwa muhula wa sita kwa karibu 80% ya kura, kulingana na uchunguzi rasmi.

Matangazo ya kibiashara

Mara tu baada ya kutangazwa mshindi kwa kura karibu 80%, watu walikusanyika katika mji mkuu, Minsk, ambapo kumeshuhudiwa makabiliano na polisi.

Uchaguzi huo ulizua mvutano mkubwa ambapo hali ya sintofahamu inaendelea kuripotiwa katika baadhi ya maeneo nchini humo, Kabla ya zoezi la upigaji kura, polisi iliwakamata wagombea urais wa upinzani na wafuasi wa Svetlana Tikhanovskaya, mpinzani mkuu wa Alexander Lukashenko, alipata 7% ya kura kulingana na tume ya uchaguzi nchini Belarus; Haliambayo ilisababisha kuzuka maandamano makubwa dhidi ya utawala.

Awali Svetlana Tikhanovskaya alitaka uchaguzi uliofanyika jana Jumapili kuwa wa haki na uwazi.

Wakati huo huo rais Lukashenko aliwaambia raia wa taifa hilo kwamba hakutatokea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Belarus kwa kuwa amejipanga kuzuia majaribio yote ya kuidhoofisha serikali yake.