HONG KONG-USALAMA-HAKI

Sheria ya usalama Hong Kong: Polisi yamshikilia mmiliki wa vyombo vya habari Jimmy Lai

Mmiliki wa vypmbo vya habari vinavyounga mkono demokrasiaJimmy Lai, katika makao makuu ya gazeti lake la Next Digital huko Hong Kong.
Mmiliki wa vypmbo vya habari vinavyounga mkono demokrasiaJimmy Lai, katika makao makuu ya gazeti lake la Next Digital huko Hong Kong. Anthony WALLACE / AFP

Jimmy Lai ni moja wapo ya viongozi wakuu wanaharakati wanaounga mkono demokrasia huko Hong Kong. Amekamatwa leo Jumatatu Agosti 10 chini ya sheria mpya ya usalama wa kitaifa, ndugu zake na chanzo cha polisi wamebaini.

Matangazo ya kibiashara

Muda mfupi baadaye, polisi kadhaa wa Hong Kong walivamia makao makuu ya gazeti lake la kila siku la Apple Daily, ambalo ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya Beijing.

"Wamemkamata nyumbani kwake karibu saa moja asubuhi huko Hong Kong [sawa na saa sita usiku saa za kimataifa]. Mawakili wetu wako njiani kwnda kituo cha polisi, "Mark Simon ameliambia shirika la habari la AFP.

Kulingana na mshirika wa karibu wa Jimmy Lai, waandishi wengine wahabari kutoka gazeti lake pia wamekamatwa. Hii ni hatua mpya ya Beijing katika kulidhibiti koloni la zamani la Uingereza.

Muda mfupi kabla, Mark Simon alitangaza kwenye mtandao wa Twitter kwamba polisi inajaribu kumkamata Jimmy Lai na kwamba maafisa wa polisi walikuwa wakifanya msako nyumbani kwake na nyumbani kwa mwanae.

Chanzo cha kipolisi ambacho kilizungumza lakini kwa sharti la kutotaja jina lake, kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba Lai alikamatwa kwa madai hayo ya kushirikiana na mataifa ya kigeni pamoja na udanganyifu. Hata hivyo, jeshi lenyewe halikuzungumzia mara moja taarifa hiyo.

Lai ni mtu wa kwanza mashuhuri kukamatwa hadi sasa chini ya sheria hiyo mpya ya usalama ya Hong Kong. Beijing ilianzisha sheria hiyo kuelekea Hong Kong mwishoni mwa mwezi Juni, kufuatia miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga serikali mwaka jana.

Lai aliwahi kukamatwa mwaka huu kwa madai ya kuandaa kusanyiko kinyume cha sheria, pamoja na washirika wenzake wanaounga mkono demokrasia, wakihusishwa na maandamano ya mwaka jana.