BELARUS-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Mwanasiasa wa upinzani Belarus Svetlana Tikhanovskaïa akimbilia Lithuania

Alexander Lukashenko anakabiliwa na upinzani kutoka kwa Svetlana Tikhanovskaya. Mke wa mwanablogi aliyefungwa ametokea kuwa maarufu nchini Belarus, akimkosoa rais aliye na mamlaka kamili na ambaye yuko madarakani kwa kipindi cha miaka 26.
Alexander Lukashenko anakabiliwa na upinzani kutoka kwa Svetlana Tikhanovskaya. Mke wa mwanablogi aliyefungwa ametokea kuwa maarufu nchini Belarus, akimkosoa rais aliye na mamlaka kamili na ambaye yuko madarakani kwa kipindi cha miaka 26. SERGEI GAPON / AFP

Mgombea wa urais kutoka kambi ya upinzani nchini Belarus Svetlana Tikhanovskaya, anayepinga kuchaguliwa tena kwa rais Alexander Lukashenko, amekimbilia nchini Lithuania, Waziri wa Mambo ya nje wa Lithuania Linas Linkevicius ametangaza Jumanne (Agosti 11).

Matangazo ya kibiashara
Belarussian President Alexander Lukashenko speaks during a meeting with the media in Minsk, Belarus December 14, 2018.
Belarussian President Alexander Lukashenko speaks during a meeting with the media in Minsk, Belarus December 14, 2018. REUTERS/Vasily Fedosenko

"Amewasili Lithuania na yuko salama," Linas Linkevicius amesema, wakati maandamano dhidi ya ushindi wa rais wa Belarus, aliyechaguliwa kwa muhula wa sita, yametawanywa na polisi kwa usiku wa pili mfululizo.

Hayo yanajiri wakati Umoja wa Ulaya umetilia mashaka matokeo ya uchaguzi nchini humo.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, ameitaka Belarus kutoa matokeo sahihi ya uchaguzi wa rais, baada ya rais Alexander Lukashenko kuibuka na ushindi mkubwa.

Rais Lukashenko ameshinda uchaguzi wa rais kwa asilimia 80 ya kura na kupongezwa na jirani yake, Rais wa Urusi Vladmir Putin, lakini mataifa kadhaa ya Magharibi yameonyesha wasiwasi juu ya ushindi wake.

Awali rais Lukashenko aliwaambia raia wa taifa hilo kwamba hakutatokea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Belarus kwa kuwa amejipanga kuzuia majaribio yote ya kuidhoofisha serikali yake.