BELARUS-POLAND-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Belarus: Poland yapendekeza kuwa mpatanishi baada ya uchaguzi wa urais kupingwa

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki alikuwa wa kwanza kuitisha mkutano wa dharura wa umoja wa Ulaya baada ya uchaguzi nchini Belarus. Poland sasa imependekeza kuwa mpatanishi ili kutuliza mzozo Belarus.
Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki alikuwa wa kwanza kuitisha mkutano wa dharura wa umoja wa Ulaya baada ya uchaguzi nchini Belarus. Poland sasa imependekeza kuwa mpatanishi ili kutuliza mzozo Belarus. STEPHANIE LECOCQ / POOL / AFP

Wakati viongozi mbalimbali wakiendelea kulaani machafuko ya wanamgambo wa Belarus dhidi ya waandamanaji, Poland imependekeza kuwa mpatanishi ili kujaribu kutuliza mzozo unaoendelea nchini humo kati ya utawala na upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Mpango huu mpya unaonyesha jinsi gani msimamo wa Poland ulivyo tangu uchaguzi wa urais nchini Belarus.

Siku moja baada ya uchaguzi wa urais nchini Belarus, Mateusz Morawiecki, Waziri Mkuu wa Poland amekuwa wa kwanza kuitisha mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya.

Wazo la upatanishi lilifuata saa chache baadaye, baada ya kupendekezwa kwanza na naibu waziri wa mambo ya nje na kisha kurudiwa na waziri wa mambo ya nje wa Poland, Jacek Czaputowicz.

Wito wake ameutoa baada ya siku mbili za maandamano kutokea kufuatia uchaguzi uliogubikwa na utata.

Hayo yanajiri wakati mpinzani mkuu katika uchaguzi wa Belarus Svetlana Tikhanovskaya yuko ukimbizini nchini Lithuania. Bi Tikhanovskaya amesema alifanya maamuzi magumu ya kuondoka nchini humo baada ya makabiliano kuibuka kati ya polisi na waandamanaji yaliyosababisha kifo cha mwandamanaji mmoja.

Tikhanovskaya ambaye anadai kuwa alishinda uchaguzi huo, amesema aliamua kuondoka nchini humo na kutafuta hifadhi Lithuania kutokana na usalama wa watoto wake.