HONG KONG-USALAMA-HAKI

Hong Kong: Jimmy Lai atoa wito kwa wanahabari wake kuendelea kupambana

Mwanaharakati wa demokrasia na mfanyibiashara maarufu  katika eneo la Hong Kong Jimmy Lai.
Mwanaharakati wa demokrasia na mfanyibiashara maarufu  katika eneo la Hong Kong Jimmy Lai. AFP PHOTO / Philippe Lopez

Mwanaharakati wa demokrasia na mfanyibiashara maarufu  katika eneo la Hong Kong Jimmy Lai ameachiliwa huru na kuwatolea wito waandishi wake wa habari kuendelea kupambana.

Matangazo ya kibiashara

Jimmy Lai alikamatwa chini ya sheria ya usalama wa kitaifa kwa madai ya kushirikiana kwa karibu na mataifa ya kigeni kuhamasisha maandamano katika eneo hilo.

"Tuendelea na mapambano, tuendelea kupambana," Jimmy Lai amewaambia waandishi wa habari wa Gazeti la Apple Daily, kulingana na video iliyorushwa moja kwa moja kwenye Facebook, kabla ya kuongeza: "Tunaungwa mkono na wa wakazi wa Hong Kong, hatuwezi kuwakatisha tamaa ”.

Lai amekuwa maarufu katika harakati za kuunga mkono maandamano yanayohimiza mageuzi, kutaka uhuru wa watu wa Hong Kong kujitawala na kutoinga sheria mpya za usalama.

Hii sio mara ya kwanza kwa mfanyabishara huyo mwenye umri wa miaka 71 kukamatwa. Mwezi Februari alitiwa mbaroni kwa madai ya kukosa la kushiriki katika mkusanyiko uliopigwa marufu lakini akaachiwa kwa dhamana.

Sheria mpya ya usalama katika eneo hilo linaipa mamlaka China, kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wanaharakati na wapinzani wa uongozi wa Beijing kwa madai ya kutishia usalama wake.