BELARUS-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Belarus: Waandamanaji 700 wakamatwa baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais

Nchini Belarus, wanawake waliovaa nguo za rangi nyeupe wanaomba ndugu zao ambao wamepigwa na polisi waachiliwe huru mara moja.
Nchini Belarus, wanawake waliovaa nguo za rangi nyeupe wanaomba ndugu zao ambao wamepigwa na polisi waachiliwe huru mara moja. Sergei GAPON / AFP

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Belarus imetangaza kwamba watu 700 wanazuliwa tangu Jumatano wiki hii, siku ya nne ya maandamano ya kabla ya uchaguzi mkuu, na kufanya jumla ya watu waliokamatwa kufikia kufikia 6,700.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo kadhaa kutoka mashirika ya kiraia, vikosi vya usalama vitlitulia nguvu nyingi kupita kiasi kwa kuzima maandamano hayo.

"Watu wengi hawashiriki tena katika machafuko. Lakini kiwango cha mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama kimeendelea kuongezeka, " imesema idara ya habari ya wizara ya Mambo ya Nadani imebaini kwenye akaunti yake ya Telegraph.

Wiki hii Poland ilipendekeza kuwa mpatanishi ili kujaribu kutuliza mzozo unaoendelea nchini Belarus kati ya utawala na upinzani.

Hayo yanajiri wakati mpinzani mkuu katika uchaguzi wa Belarus Svetlana Tikhanovskaya yuko ukimbizini nchini Lithuania. Bi Tikhanovskaya amesema alifanya maamuzi magumu ya kuondoka nchini humo baada ya makabiliano kuibuka kati ya polisi na waandamanaji yaliyosababisha kifo cha mwandamanaji mmoja.

Tikhanovskaya ambaye anadai kuwa alishinda uchaguzi huo, amesema aliamua kuondoka nchini humo na kutafuta hifadhi Lithuania kutokana na usalama wa watoto wake.