URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi nchini Urusi yapindukia zaidi ya 907,000

Sampuli za chanjo ya Corona iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti ya Gamaleya, huko Moscow, Urusi, Agosti 6, 2020.
Sampuli za chanjo ya Corona iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti ya Gamaleya, huko Moscow, Urusi, Agosti 6, 2020. The Russian Direct Investment Fund (RDIF)/Handout via REUTERS

Mamlaka ya afya nchini Urusi imeandikisha visa vipya 5,057 vya maambukizi ya Corona na vifo vipya 124 katika muda wa saa 24 zilizoopita.

Matangazo ya kibiashara

Pamoja na jumla ya idadi ya visa 907,758 vya maambukizi , Urusi ni nchi ya nne duniani iliyoathirika zaidi na janga la Covid-19 kwa suala la maambukizi.

Ugojnwa huo hatari wa Covid-19 pia umesababisha vifo vya watu 15,384 nchini Urusi.

Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani, WHO, lilionya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.

WHO imeendelea kukosoa hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na baadhi ya nchi duniani kwa kulegeza masharti ya kukabiliana na janga la Covid-19, ikisema kuwa Covid-19 bado ni tishio duniani.