Belarus yawaachilia waandamanaji kabla ya EU kuchukua vikwazo
Mamlaka ya Belarus imechukuwa hatua ya kuwaachilia huru waandamanaji waliyokamatwa wakati wa maandamano katika siku za hivi karibuni baada ya kuomba msamaha kwa umma.
Imechapishwa:
Hata hivyo hasira ya waandamanaji ni changamoto kubwa inayomkabili Rais aliyechaguliwa Alexander Lukashenko, ambaye yuko madarakani kwa miaka 26.
Hatua hii ya kuawaachilia huru waandamanaji hawa inakuja saa chache kabla ya mkutano wa mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya, ambao wanaweza kujadili vikwazo vipya dhidi ya viongozi wa Belarus, wakichukuliwa kitendo cha vikosi vya usalama kuwakandamiza waandamanaji.
Belarusi iko tayari kwa mazungumzo "ya kujenga na yenye malengo" juu ya matukio yanayohusiana na uchaguzi wa urais, Waziri wa Mambo ya nje wa Belarus Vladimir Makei akinukuliwa na shirika la habari la BeITA amesema leo asubuhi.