BELARUS-MAANDAMANO-SIASA-USALAMA

Maandamano yaendelea Belarus, Lukashenko aapa kusalia madarakani

Makumi ya maelfu ya wafuasi wa upinzai wa Belarus wamekusanyika Minsk Agosti 16, 2020, kujiunga na "maandamano ya uhuru".
Makumi ya maelfu ya wafuasi wa upinzai wa Belarus wamekusanyika Minsk Agosti 16, 2020, kujiunga na "maandamano ya uhuru". Sergei GAPON / AFP

Maelfu ya waandamanaji wa upinzani wameandamana jiji Minks nchini Belarus kumshinikiza rais Alexander Lukashenko kujiuzulu kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wanayosema hayakuwa huru na haki.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya yameelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa ndio makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo hivi karibuni.

Watu wanaoakadiriwa kuwa zaidi ya Laki Moja, walikusanyika katika uwanja wa uhuru wakiimba nyimbo na kuwa na mabango ya kumshutumu rais Lukashenko kama kiongozi muuaji na mnyanyasaji.

Hata hivyo, maandamano hayo yanaonekana kutomtisha rais Lukashenko ambaye naye aliongoza mkutano wa wafuasi wake na kuwafananinisha wapinzani wake kama panya.

Mgombea mkuu wa upinzani Svetlana Tikhanovskaya aliyepambana na Lukashenko aliyetangzwa mshindi wa Uchaguzi huo kwa kupata asilimia 80, aliitisha maandamano hayo baada ya kukimbilia katika nchi jirani ya Lithuania.

Maandamano zaidi na migomo inatarajiwa kushuhudiwa wiki hii, wakati huu upinzani ukiendelea kusisitiza kuwa rais Lukashenko aliiba kura na kupewa ushindi usiokuwa halali.