BELARUS-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Rais wa Belarus Lukashenko anyooshea kidole cha lawama upinzani

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko wakati wa hotuba yake mbele ya wafuasi wake Agosti 16, 2020.
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko wakati wa hotuba yake mbele ya wafuasi wake Agosti 16, 2020. Siarhei LESKIEC / AFP

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ameushtumu upinzani kwa kujaribu kufanya mapinduzi kwa kutumia vurugu wakati nchi hiyo ikiendelea kukumbwa na uhasama unaotokana na kupingwa kwa matokeo ya uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Upinzani umepinga matokeo ya uchaguzi ambapo rais Lukashenko alipata asilimia 80 ya kura zilizopigwa.

Mapema wiki hii rais wa Belarus Alexander Lukashenko aliahidi kwamba uchaguzi mpya wa urais utafanyika baada ya marekebisho ya katiba.

Rais Alexander Lukashenko, ambaye ushindi wake katika uchaguzi wa urais wa hivi karibuni umeendelea kuzua maandamano makubwa ameonekana akinyooshea kidole cha lawama upinzani akisema kuwa unajaribu kutumia raia kwa kuzusha vurugu nchini.

Maandamano yameongezeka nchini Belarus ili kumshinikiza rais Lukashenko aachie ngazi.