INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Karibu kesi zaidi ya 70,000 zathibitishwa nchini India

India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo kwa idadi ya maambukizi baada ya Marekani na Brazil.
India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo kwa idadi ya maambukizi baada ya Marekani na Brazil. REUTERS

India imerekodi kesi mpya 78,672 za maambukizi ya virusi vya Corona zilizothibitishwa, rekodi ya siku moja ambayo inafanya idadi ya visa vya maambukizi kufikia Milioni 2.84 nchini humo, kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Afya ya India.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo imeongezeka hadi 53,886, na watu 997 wamefariki dunia katika saa ishirini na nne zilizopita.

India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo kwa idadi ya maambukizi baada ya Marekani na Brazil.

Kufikia sasa zaidi ya watu milioni 22 wameambukizwa virusi vya Corona ulimwenguni, kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins, huku watu 788, 000 wakithibitishwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.