MAREKANI-CHINA-HON KONG-USHIRIKIANO

Marekani yasitisha mikataba 3 ya pande mbili na Hong Kong, China yajibu

Donald Trump mwezi uliopita aliamuru utawala wake kusitisha huduma na misaada mingine iliyokuwa inapewa Hong Kong ili kuiadhibu China kwa kile rais wa Marekani alielezea kama vitendo vya 'ukandamizaji' dhidi ya koloni la zamani la Uingereza.
Donald Trump mwezi uliopita aliamuru utawala wake kusitisha huduma na misaada mingine iliyokuwa inapewa Hong Kong ili kuiadhibu China kwa kile rais wa Marekani alielezea kama vitendo vya 'ukandamizaji' dhidi ya koloni la zamani la Uingereza. DALE DE LA REY / AFP

Wizara ya mambo ya nje wa Marekani imeiarifu Hong Kong juu ya kusitishwa kufutwa kwa mikataba mitatu ya pande mbili, kwa kujibu mpango wa China, wa kuweka sheria mpya ya usalama wa kitaifa kwa Hong Kong.

Matangazo ya kibiashara

Marekani inaona kuwa sheria hiyo inkkuja kukandamiza uhuru wa wakazi wa Hongo Kong.

Wakati huo huo China kupitia wizara ya mambo ya nje imesema saa kadhaa baadaye kwamba koloni hilo la zamani la Uingereza litasitisha baadhi ya mikataba ya ushirikiano wa mahakama na Marekani.

Donald Trump mwezi uliopita aliamuru utawala wake kusitisha huduma na misaada mingine iliyokuwa inapewa Hong Kong ili kuiadhibu China kwa kile rais wa Marekani alielezea kama vitendo vya 'ukandamizaji' dhidi ya koloni la zamani la Uingereza.

Katika taarifa, wizara ya mambo ya nje wa Marekani imesema mikataba inayohusika inahusu "kukabidhiana wahalifu wanaotoka katika nchi moja kwenda nyingine, kukabidhiana watu waliohukumiwa kutoka nchi moja kwenda nyingine kati ya nchi hizo mbili na msamaha wa ushuru wa mapato yanayopatikana kutoka kwa matumizi ya kimataifa ya meli.

"Hatua hizo zinasisitiza 'wasiwasi mkubwa' wa Washington juu ya uamuzi wa Beijing wa kuweka sheria ya usalama wa kitaifa ambayo "ilifuta uhuru wa raia wa Hong Kong," msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Morgan Ortagus amesema.

Hizi ni hatua ambazo zinaonekana kama njia ya "kuchochea vurugu katika uhusiano kati ya China na Marekani, kwa kutumia Hong Kong kama kibaraka," serikali ya China imebaini.