Belarus: Utawala wajaribu kuminya upinzani
Jaribio la kuzima maandamano linaendelea nchini Belarusi. Mamlaka imetangaza kufungua kesi ya jinai dhidi ya wanaharakati wa upinzani ambao walianzisha baraza la kujadiliana kuhusu mabadiliko ya kidemokrasia wakati maandamano makubwa ya kupinga matokeo ya uchaguzi yakiendelea.
Imechapishwa:
Wakati huo huo wakili wa aliye kuwa mgombea urais kutoka kambi ya Svetlana Tikhanovskaya ametakiwa kuripoti leo Ijumaa asubuhi mbe ya ofisi ya maafisa wa wachunguzi.
Viongozi wa 'kamati ya uratibu' wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 5 jela. Wanashtumiwa kutaka kuendelea serikali ya mpito baada ya uchaguzi wa rais Agosti 9 ambao uliibua mvutano kubwa na kusababisha maandamano makubwa nchini humo.
Hayo yanajri wakati rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na kiongozi wa Ujerumani, Kansela Angela Merkel wamejitolea kusuluhisha mzozo wa uchaguzi nchini Belarus.
Wawili hao wakizungumza baada ya mkutano wa Umoja wa Ulaya, wamesema hawatambui ushindi wa rais Alexander Lukashenko.
Wakati huo huo Rais wa Urusi, Vladimir Putin amemwambia rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel kwamba shinikizo lolote kwa uongozi wa Belarus au uingiliaji wa nje katika masuala ya ndani ya nchi hiyo halina faida. Matamshi hayo ameyatoa katika mazungumo yake na Charles Michel yaliyofanyika kwa njia ya simu.
Hata hivyo pande hizo mbili zimekubaliana kwamba kuituliza mapema hali ya Belarus ni njia inayofaa kwa maslahi ya Urusi na Umoja wa Ulaya.