URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yazidi 960,000 nchini Urusi

Sampuli za chanjo ya Corona iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti ya Gamaleya, huko Moscow, Urusi, Agosti 6, 2020.
Sampuli za chanjo ya Corona iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti ya Gamaleya, huko Moscow, Urusi, Agosti 6, 2020. The Russian Direct Investment Fund (RDIF)/Handout via REUTERS

Urusi imerekodi visa vipya 4,744 vya maambukizi ya virusi vya Corona, na kufanya idadi hiyo kufikia 961,493 na kuifanya nchi hiyo kuwa nchi ya nne iliyoathirika zaidi katika suala la maambukizi.

Matangazo ya kibiashara

Urusi pia imeripoti vifo vipya 65 katika saa 24 zilizopita na idadi ya vifo sasa imefikia 16,448 tangu kuzuka kwa janga hilo.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Tayari virusi hivyo vimesambaa katika mabara yote duniani.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Wiki iliyopita Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema linatumai kwamba janga la Corona linaweza kuwa limemalizika kabisa katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Itachukuwa miaka miwili kumalizika kabisa kwa homa ya Uhispania, ambayo ilizuka mnamo mwaka 1918, Tedros Adhanom Ghebreyesus alikumbusha.

Zaidi ya watu milioni 23 duniani wameambukizwa ugonjwa wa Covid-19 na watu 809,000 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo hatari, kulingana na takwimu za taasisi ya Robert Koch (RKI)