UFILIPINO-USALAMA

Ufilipino: Kumi waangamia katika mashambulizi mawili Jolo

Askari wakisafirisha wahanga wa mashambulizi mawili huko Jolo, Ufilipino, Agosti 24, 2020.
Askari wakisafirisha wahanga wa mashambulizi mawili huko Jolo, Ufilipino, Agosti 24, 2020. AFP

Watu wasiopunguwa kumi wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi mawili yaliyotokea leo Jumatatu katika kisiwa cha Jolo, ngome ya kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Abu Sayyaf, Kusini mwa Ufilipino.

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi watano na raia wanne wameuawa katika mlipuko wa kwanza karibu na duka kubwa katika mji wa Jolo baada ya bomu lililotengenezwa kienyeji na kutegwa kwenye pikipiki kulipuka, Jenerali Corleto Vinluan amewaambia waandishi wa habari.

Askari 16 pia wamejeruhiwa katika mlipuko huo ambao umetokea leo mchana. Takriban raia 20 pia wamejeruhiwa, Luteni Kanali Ronaldo Mateo amesema, akinukuu meya wa jiji hilo.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga baadaye alilipua mkanda wake uliojaa vilipuzi katika mtaa kulikotokea shambulio la kwanza wakati polisi ilikuwa ikijaribu kuondoa watu kwenye eneo hilo. Mlipuko huo umesababisha mtu mmojakupoteza maisha na kujeruhi maafisa sita wa polisi, Vinluan amesema.

Kisiwa hicho cha Jolo chenye Waislamu wengi ni ngome ya kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Abu Sayyaf, lililogawanyika kwa makundi kadhaa, ambayo baadhi yana mafungamano na kundi la Islamic State (IS).

Kundi la Abu Sayyaf linachukuliwa na Washington kama kundi la kigaidi na Washington.

kundi la Abou Sayyaf linajihusisha hasa na vitendo vya utekaji nyara raia.